Pilikapilika
Wednesday, October 5, 2011
Tuesday, September 27, 2011
Mrembo aolewa na mbwa Ghana..
A Ghanaian woman has married her dog because it has qualities she had seen only in her late father. Emily Mabou, 29, of Aburi, married the 18-month-old dog in a ceremony attended by a traditional priest and local, curious villagers, reports the Daily Dose.
Her younger brother David Mabou said her family boycotted the wedding which they felt was “a stupid step to combat her loneliness”.But Ms Mabou said: “For so long, I’ve been praying for a life partner who will have all the qualities of my dad. My dad was kind, faithful, and loyal to my mum, and he never let her down.
“I’ve been in relationships with so many men…, and they are all the same… skirt-chasers and cheaters. My dog is kind, and loyal to me and he treats me with so much respect.”

In the ceremony, the priest warned villagers not to mock the wedding, but to “rejoice with her as she has found happiness at last”.
ananova.com

Sunday, September 25, 2011
.....Mtoto wa Kike afanyiwa UNYAMA...!
Serikali na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za wanawake na watoto nchini Tanzania imeingilia kati sakata la tukio la mtoto wa miaka 14 kufanyiwa unyama wa kubakwa na watu 16. Katika hali inayoenekana kuguswa na tukio hilo, Serikali kupitia ofisi ya Mkurugenzi wa makosa ya jinai (DPP) imeamua kupitia upya faili la maelezo kutoka Jeshi la Polisi ili kuainisha na kesi iliyopelekwa mahakamani.
Taasisi nyingine zilizoingilia suala hilo ni Chama cha Waandishi wa Habari wanawake (TAMWA) na Shirika linalosadia watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (PASADA) ambapo kwa pamoja zimechukua hatua ya kumpeleka mtoto huyo hospitali kwa ajili ya kupata matibabu.
Mtoto huyo (Jina linahifadhiwa) anayesoma darasa la nne, alibakwa na idadi hiyo ya watu kwa saa mbili mfululizo wakati akirudi kutoka kwa mwalimu wake wa maigizo nya
kati za usiku.
Hata hivyo watu watatu kati ya 10 wanaotuhumiwa katika tukio hilo wamefikishwa kwenye mahakama ya Wilaya ya Temeke kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo.Watu hao ni Yusuph Bakari (25), Abdul Salumu (17) na Omari Mkuu (16), wote wakazi wa Nzasa.
Akizungumza na gazeti hili, wakili wa Serikali kutoka ofisi za DPP, Lucy Uiso alisema licha ya suala hilo kufikishwa mahakamani lakini wao wana wajibu wa kufuatilia kwa karibu kuhakikisha watu hao wamefunguliwa kesi kulingana na uzito wa tukio.Alisema baada ya kumuona mtoto huyo, wamejiridhisha amefanyiwa kitendo cha kinyama kiasi ambacho kimemuacha akiwa kwenye mateso makubwa, "Tumetoka huko kumuona yule mtoto, ana hali mbaya sana na sisi tunachokifanya ni kwenda kuangalia faili la polisi ili kuoanisha kama maelezo yanakwenda na uzito wa tukio," alisema Uiso.

Kauli hiyo ya Mwanasheria wa serikali imeonekana kutekelezwa baada ya mfanyakazi wa mahakama hiyo (Jina hakutaka litajwe) kukiri kuwa jalada la kesi hiyo limechukuliwa na ofisi hiyo toka mwanzoni wa wiki kwa ajili ya kupitiwa.Akizungumza na gazeti hili Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Ananilea Nkya, alisema wameguswa na tukio hilo na chama chake kimefanya juhudi za kumpeleka mtoto huyo hospitali baada ya wazazi wake kukosa pesa za kumpeleka, "Kitu cha kwanza ni kuwasiliana na madaktari wa Hospitali ya Temeke kwa ajili ya kumpeleka pale apatiwe matibabu, mengine tutaiachia mahakama iendelee na kazi yake," alisema Nkya.
Habari zilizopatikana zinaeleza tayari mtoto huyo amefikishwa Hospitali ya Temeke kwa msaada wa PASADA na kupatiwa matibabu ya awali pamoja na vipimo mbalimbali vya kuchunguza afya yake.Mama mzazi wa binti huo (jina linahifadhiwa) alisema alifikishwa Hospitalini hapo siku ya Jumanne kwa msaada wa PASADA, "Nashukuru wanasheria wa Serikali, TAMWA na PASADA kwa kunifikisha hapa nilipo, nafurahi mtoto wangu amepatiwa matibabu na hivi sasa hali yake imeanza kubadilika na kuwa nzuri," alisema.
Alisema kutokana na matibabu hayo, hali ya kutokwa na damu pamoja na usaha katika sehemu zake za siri imeanza kukatika na ameanza kutembea vizuri tofauti na mwanzo.
Katika tukio hilo lilotokea Agosti 31, mwaka huu, binti huyo alieleza alibakwa na kundi la watu 16 mara baada ya kukamatwa kwa nguvu na walipomaliza haja zao walitaka kumtumbukiza ndani ya kisima ili afe na maji.
source: http://www.wavuti.com
Taasisi nyingine zilizoingilia suala hilo ni Chama cha Waandishi wa Habari wanawake (TAMWA) na Shirika linalosadia watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (PASADA) ambapo kwa pamoja zimechukua hatua ya kumpeleka mtoto huyo hospitali kwa ajili ya kupata matibabu.
Mtoto huyo (Jina linahifadhiwa) anayesoma darasa la nne, alibakwa na idadi hiyo ya watu kwa saa mbili mfululizo wakati akirudi kutoka kwa mwalimu wake wa maigizo nya
kati za usiku.Hata hivyo watu watatu kati ya 10 wanaotuhumiwa katika tukio hilo wamefikishwa kwenye mahakama ya Wilaya ya Temeke kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo.Watu hao ni Yusuph Bakari (25), Abdul Salumu (17) na Omari Mkuu (16), wote wakazi wa Nzasa.
Akizungumza na gazeti hili, wakili wa Serikali kutoka ofisi za DPP, Lucy Uiso alisema licha ya suala hilo kufikishwa mahakamani lakini wao wana wajibu wa kufuatilia kwa karibu kuhakikisha watu hao wamefunguliwa kesi kulingana na uzito wa tukio.Alisema baada ya kumuona mtoto huyo, wamejiridhisha amefanyiwa kitendo cha kinyama kiasi ambacho kimemuacha akiwa kwenye mateso makubwa, "Tumetoka huko kumuona yule mtoto, ana hali mbaya sana na sisi tunachokifanya ni kwenda kuangalia faili la polisi ili kuoanisha kama maelezo yanakwenda na uzito wa tukio," alisema Uiso.
Kauli hiyo ya Mwanasheria wa serikali imeonekana kutekelezwa baada ya mfanyakazi wa mahakama hiyo (Jina hakutaka litajwe) kukiri kuwa jalada la kesi hiyo limechukuliwa na ofisi hiyo toka mwanzoni wa wiki kwa ajili ya kupitiwa.Akizungumza na gazeti hili Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Ananilea Nkya, alisema wameguswa na tukio hilo na chama chake kimefanya juhudi za kumpeleka mtoto huyo hospitali baada ya wazazi wake kukosa pesa za kumpeleka, "Kitu cha kwanza ni kuwasiliana na madaktari wa Hospitali ya Temeke kwa ajili ya kumpeleka pale apatiwe matibabu, mengine tutaiachia mahakama iendelee na kazi yake," alisema Nkya.
Habari zilizopatikana zinaeleza tayari mtoto huyo amefikishwa Hospitali ya Temeke kwa msaada wa PASADA na kupatiwa matibabu ya awali pamoja na vipimo mbalimbali vya kuchunguza afya yake.Mama mzazi wa binti huo (jina linahifadhiwa) alisema alifikishwa Hospitalini hapo siku ya Jumanne kwa msaada wa PASADA, "Nashukuru wanasheria wa Serikali, TAMWA na PASADA kwa kunifikisha hapa nilipo, nafurahi mtoto wangu amepatiwa matibabu na hivi sasa hali yake imeanza kubadilika na kuwa nzuri," alisema.
Alisema kutokana na matibabu hayo, hali ya kutokwa na damu pamoja na usaha katika sehemu zake za siri imeanza kukatika na ameanza kutembea vizuri tofauti na mwanzo.
Katika tukio hilo lilotokea Agosti 31, mwaka huu, binti huyo alieleza alibakwa na kundi la watu 16 mara baada ya kukamatwa kwa nguvu na walipomaliza haja zao walitaka kumtumbukiza ndani ya kisima ili afe na maji.
source: http://www.wavuti.com
Saturday, September 24, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)